03-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Kumfanyia Hajj Aliyekuwa Kilema

SWALI:
 
Nina mtoto kilema ambaye namfikiria kuwa akifanya Hajj mwenyewe nakhofu kuwa atataabika na kupata madhara. Hivyo je, naweza kumfanyia Hajj?

 

JIBU:

Ikiwa mtoto ni kilema kama unavyosema, basi inaruhusiwa kumfanyia fardhi ya Hajj ikiwa wewe mwenyewe umeshafanya fardh ya Hajj.

 
[Liqa-aat al-Baab al-Maftuwh – Mjalada 1, Uk. 45, Namba 67]