Shaykh Swaalih Al-Fawzaan: Anayeacha Swiyaam Ramadhwaan Juu Ya Kuwa Hapingi Kuwajibika Kwake

SWALI:
 
Mwenye kuacha Swiyaam ya Ramadhwaan lakini hapingi kuwajibika kwake je anakufuru kwa hilo? 
 
JIBU:
 
Ndio. Vipi ataacha Swiyaam na wakati huo hapingi? Vipi ataacha Swawm ya Ramadhwaan naye hana udhuru unaomruhusu ki-Shariy’ah ikiwa kweli hapingi? Ameacha kwa kuwa anaona si waajib:
 
[Fataawa Ramadhwaan Shaykh Fawzaan]