Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Kujipaka Au Kunusa Mafuta Mazuri Akiwa Katika Swawm

SWALI:
 
Nini hukumu ya mtu aliyefunga na kutumia mafuta mazuri siku za Ramadhaan?
 
JIBU:
 
Hakuna ubaya kutumia na kunusa mafuta mazuri siku za Ramadhwaan isipokuwa kufukiza bukhuwr (udi) usikaribie hadi ukavuta pumzi za moshi na ukaingia tumboni.
 
[Imaam Muhammad bin Swaalih Ibn ‘Uthyamiyn - Fiqhul ‘Ibaadaat Uk. No. 217 Maktabatul-Iymaan]