Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Israfu Ya Chakula Wakati Wa Futari

SWALI:
 
Je, mtu hupata thawabu ndogo (ya Swawm) ikiwa atakithirisha kukata Swawm (Futari) kwa masahani ya vyakula mbali mbali?
 
JIBU:
 
Hapana, hupati thawabu ndogo ya Swawm. Mtu kufanya kitendo cha haraam baada ya kumaliza Swawm, (kitendo kile) hakiathiri thawabu (za Swawm). Bali inaingia katika neno Lake Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
وَكُلُوا وَاشْرَبُوا وَلَا تُسْرِفُوا ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْرِفِينَ ﴿٣١﴾
“Na kuleni na kunyweni; na wala msifanye israfu. Hakika Yeye (Allaah) Hapendi wanaofanya israfu. [Al-A’raaf 7: 31]
 
Huku kufanya israfu ndiyo haraam. Na iktisadi ni nusu ya maisha. Ikiwa bila kukusudia kutabaki chakula, ni afadhali kitolewe swadaqah.
 
 
[Fiqhu Al-'Ibaadah, uk. 252]