Imaam Ibn Qudaamah Al-Maqdisiy: Mwanamke Anayelazimishwa Kujimai Wakati Wa Ramadhwaan

SWALI:
 
Ikiwa mwanamke atalazimishwa jimai, halazimiki kulipa kafara, bali analazimika kulipa tu siku hiyo?
 
JIBU:
 
 Muhannaa kasema: "Nilimuuliza Ahmad kama mwanamke aliyebakwa analazimika kulipa siku hiyo. Akasema: "Ndiyo." Pia nikamuuliza kama analazimika kulipa kafara, akasema: "Hapana!"
 
Maoni haya anakubaliana nayo pia al-Hasan, Ath-Thawriy, Al-Awza'iy na Hanafiyyah. 
 
Kulingana na swali hili, inamuhusu pia mwanamke ambaye kaingiliwa wakati amelala.
 
Maalik kasema kuhusiana na mwanamke aliyelala: "Ni juu yake kulipa siku hiyo, ila hatolipa kafara. Ama kuhusiana na mwanamke ambaye amelazimishwa kujimai, analazimika kulipa siku hiyo na kutoa kafara.”
 
Ash-Shaafi'iy, Abuu Ath-Thawriy na Ibnul-Mundhir wanasema ikiwa ataingiliwa jimai kwa matisho, basi wana maoni sawa na sisi.
 
[Al-Mughniy (4/376) Daar 'Alaam-il-kutub, 1419/1999]